Wednesday, July 6, 2011

VIKO PHARM FC WAKARIBIA KUPANDA DARAJA






Kikosi cha viko pharm fc kina karibia kupanda daraja baada ya kumaliza mzunguko wa raundi kumi na moja na kushika nafasi ya pili, katika kufanikiwa kushika nafasi ya pili viko pharm mechi zote zilikuwa kumi na imeshinda mechi tano, imetoa droo mechi nne na kufungwa mechi moja na kumaliza ikiwa katika msimamo na kuchukuwa nafasi ya pili.
Katika mechi hizo viko pharm imeshinda magoli ishirini na  mbili na kufungwa magoli kumi. 
Hivi sasa viko pharm inasubiri mechi moja ambayo itaamua hatima yao ya kupanda au kubakia katika daraja hilo hilo, utaratibu uliopo sasa ni kuwa kuna makundi mawili ambayo kila kundi linajumuisha timu kimi na moja na kila kundi linatoa timu mbili za juu na ambapo mshindi wa kwanza wa kila kundi anapanda daraja moja kwa moja na mshindi wa pili wa kundi A na mshindi wa pili wa kundi B watacheza pamoja kutafuta mshindi ambaye atajumuisha timu tatu zitakazo panda daraja la kwanza kwa msimu mpya unaoanza mwezi wa septemba.
Hivi sasa viko pharm inasubiri kukamilisha mechi ili ianze kujiandaa na msimu mpya wa ligi na katika matayarisho hayo imepanga kufanya safari ya matembezi Dar es salaaam ili kuweza kucheza mechi za kujiandaa na msimu. katika safari hiyo viko pharm fc itaondoka na wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza pamoja  na viongozi wake na moja ya mechi hizo za kirafiki ilizopanga kucheza ni AZAM FC ambayo imechaguliwa ili kuweza kupata mazoezi mazuri kutokana na timu hiyo kuwa na mfumo sawa na viko pharm pamoja na kuwa na mipango inayofanana katika kuendesha timu zao ikiwa ni pamoja na malengo yanayo fanana.

Juu ni kikosi cha viko pharm fc katika moja ya mechi ilizocheza msimu huu.