Wednesday, July 6, 2011

VIKO PHARM FC WAKARIBIA KUPANDA DARAJA






Kikosi cha viko pharm fc kina karibia kupanda daraja baada ya kumaliza mzunguko wa raundi kumi na moja na kushika nafasi ya pili, katika kufanikiwa kushika nafasi ya pili viko pharm mechi zote zilikuwa kumi na imeshinda mechi tano, imetoa droo mechi nne na kufungwa mechi moja na kumaliza ikiwa katika msimamo na kuchukuwa nafasi ya pili.
Katika mechi hizo viko pharm imeshinda magoli ishirini na  mbili na kufungwa magoli kumi. 
Hivi sasa viko pharm inasubiri mechi moja ambayo itaamua hatima yao ya kupanda au kubakia katika daraja hilo hilo, utaratibu uliopo sasa ni kuwa kuna makundi mawili ambayo kila kundi linajumuisha timu kimi na moja na kila kundi linatoa timu mbili za juu na ambapo mshindi wa kwanza wa kila kundi anapanda daraja moja kwa moja na mshindi wa pili wa kundi A na mshindi wa pili wa kundi B watacheza pamoja kutafuta mshindi ambaye atajumuisha timu tatu zitakazo panda daraja la kwanza kwa msimu mpya unaoanza mwezi wa septemba.
Hivi sasa viko pharm inasubiri kukamilisha mechi ili ianze kujiandaa na msimu mpya wa ligi na katika matayarisho hayo imepanga kufanya safari ya matembezi Dar es salaaam ili kuweza kucheza mechi za kujiandaa na msimu. katika safari hiyo viko pharm fc itaondoka na wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza pamoja  na viongozi wake na moja ya mechi hizo za kirafiki ilizopanga kucheza ni AZAM FC ambayo imechaguliwa ili kuweza kupata mazoezi mazuri kutokana na timu hiyo kuwa na mfumo sawa na viko pharm pamoja na kuwa na mipango inayofanana katika kuendesha timu zao ikiwa ni pamoja na malengo yanayo fanana.

Juu ni kikosi cha viko pharm fc katika moja ya mechi ilizocheza msimu huu.


Friday, June 10, 2011

USAJILI WA ARSENAL
















Klabu ya arsenal imefanikiwa kuwasajili wachezaji wawili mpaka sasa ambao ni mchezaji wa Lile na na kikosi cha taifa cha IVORY COAST Gervinyo pamoja na mchezaji wa West Bromwich Albion na timu ya taifa ya NIGERIA.
wachezaji wote tayari wamesha fanikiwa kufanya vipimo katika klabu hiyo ya jijini london

USAIN BOLT NA MAN UTD


Usain Bolt mkimbiza upepo wa kimataifa anaetokea nhini Jamaica amesema kuwa bado ndoto zake za kuichezea klabu ya manchesster united hazijafutika na malengo yake ni kukipiga katika klabu hiyo punde tu atakapo staafu katika mbio.
Bolt ambaye ndie mwanamme mwenye kasi zaidi mpaka sasa ambaye ameweka record juzi katika mbio za mita 100 na 200 na hivi sasa yuko mjini oslo kushindana katika mbio za mita 200na amesema kuwa bado anahitaji kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kurejea katika kasi yake ya kawaida.

PELE ASEMA NEYMAR ANAHITAJI JUHUDI ZAIDI



Kinda nyota anaechipukia kutoka brazili NEYMAR ameonywa na gwiji la soka wa taifa hilo na duniakwa jumla PELE kuwa anahitaji juhudi zaidi ili kuweza kufuata nyayo zake na asijishughulishe na kucheza na mashabiki kwani wanaweza kumpotezea malengo yake.
Pia gwiji huyo hakusita kumfagilia nyotaa huyo kwa kusema anaweza kumpita nyota wa sasa wa Argentina Leonel Messi kwani anaonesha kuwa na uwezo mkubwa pamoja na kuwa na umri mdogo wa miaka 19.
NEYMAR anahusishwa na kuwaniwa na vigogo viwili vya soka barani ulaya CHELSEA na REAL MADRID huku CHELSEA wanaonekana kuwa na nafasi nzuri ya kumnyakuwa kwani wao ndio walioonesha nia ya kumnyakuwa nyota huyo tangu msimu uliomalizika hivi karibuni.
Uwezo wa nyota huyo unaonekana kuwa mkubwa hasa kutokana na kuwa na uwezo wa kutumia miguu yote miwili tofauti na MESSI.

ERIC CANTONA KURUDI OLD TRAFFORD






Mchezaji wa zamani wa manchester united Eric Cantona anatarajiwa kurudi tena kwa mara nyengine katika klabu yake ya zamani ya old trafford baada ya miaka 13 kupita tangu alipoiacha timu hio
mchezaji huyo anatarajiwa kurudi tena katika uwanjani hapo katika mechi itakayopigwa kwa ajili ya kumuaga mchezaji mwenzake Paul Schooles mara baada ya kustaafu mpira mapema mwezi huu, lakini mara hii Eric Cantona anatarajiwa kurudi akiwa katika bench la ufundi akiwa kocha wa New York Cosmos. hata hivyo mchezaji mwenzake Paul schooles naye tayari amekubali kujiunga na bench la ufundi la timu hiyo mara baada ya kustaafu.
mfaransa huyo ambaye alipiga magoli 64 katika mechi 144 alizocheza katika timu yake hiyo ya zamani hakusita kusema kuwa ''natarajia kumpongeza mchezaji mwenzake Paul Schooles kwa muda wake wote alioutumia katika klabu hiyo kwa mafanilio makubwa nikiwa na majukumu yangu mapya nikwa kama kocha wa cosmos''.
Nae Paul Scholes hakusita kusema kuwa ''utakuwa ni usiku mkubwa kwangu mimi na kwa familia yangu baada ya kuitumikia klabu hii kwa maisha yangu yote, ila pia inaleta maana zaidi kwa mashabiki wa timu hii kwani wameonesha ukarimu na kunijali kwa muda wangu wote''

MANCHESTER WAMSAJILI ASHLEY YOUNG

Young, 25, is set to sign for Sir Alex Ferguson's side after he returns from holiday, ending his four-year spell in the Midlands. The Aston Villa winger has long been linked with a move away from the Birmingham outfit and is rumoured to have turned down a new contract at Villa Park.
The fee for the England international is thought to be around £16 million and he looks set to follow compatriot Phil Jones as United's second high-profile capture of the transfer window, although the deal for the defender has hit a snag over price.
Sunderland boss Steve Bruce, who spent eight years as a player at Man Utd and is also trying to buy three of United's players, told ESPNsoccernet: ''Ashley Young is a terrific signing for Sir Alex. There are not too many naturally good wide players these days, and Young is one of the best, so he will naturally enhance the United team.
"But the fact that United are willing to spend big money, at record levels in one go for the club, shows what Manchester United are all about, they are continually evolving.
"They have lost Paul Scoles, and know Ryan Giggs cannot go on forever, but they never stand still, and the way Sir Alex is going about his business at the moment show that he means business. Once again Manchester United will be the benchmark for the new season. Can anyone catch them... well, I would doubt it."
Young scored seven goals in 34 Premier League appearances last season, in addition to scoring twice for Fabio Capello's England team.

CHWAKA FC V/S VIKOPHARM FC (1-1)


Mechi kati ya vikopharm fc iliyopigwa katika uwanja wa mao tsi tung.
ilikuwa ni mpambano uliopigwa kati ya vikopharm fc na chwaka fc ambao matokeo yalikuwa 1-1
viko pharm ni timu ambayo imeleta changamoto katika soka la zanzibar maana inaonesha ni timu ambayo imejipanga katika kuleta mapinduzi ya soka nchini Tanzania.
vikopharm fc inatoa njia kwa vilabu vyengine nchini Tanzania kuiga mfano huu kwani hii ndio njia pekee kwa vilabu vya Tanzania kuweza kufanikiwa katika soka la kimataifa.