Friday, June 10, 2011

ERIC CANTONA KURUDI OLD TRAFFORD






Mchezaji wa zamani wa manchester united Eric Cantona anatarajiwa kurudi tena kwa mara nyengine katika klabu yake ya zamani ya old trafford baada ya miaka 13 kupita tangu alipoiacha timu hio
mchezaji huyo anatarajiwa kurudi tena katika uwanjani hapo katika mechi itakayopigwa kwa ajili ya kumuaga mchezaji mwenzake Paul Schooles mara baada ya kustaafu mpira mapema mwezi huu, lakini mara hii Eric Cantona anatarajiwa kurudi akiwa katika bench la ufundi akiwa kocha wa New York Cosmos. hata hivyo mchezaji mwenzake Paul schooles naye tayari amekubali kujiunga na bench la ufundi la timu hiyo mara baada ya kustaafu.
mfaransa huyo ambaye alipiga magoli 64 katika mechi 144 alizocheza katika timu yake hiyo ya zamani hakusita kusema kuwa ''natarajia kumpongeza mchezaji mwenzake Paul Schooles kwa muda wake wote alioutumia katika klabu hiyo kwa mafanilio makubwa nikiwa na majukumu yangu mapya nikwa kama kocha wa cosmos''.
Nae Paul Scholes hakusita kusema kuwa ''utakuwa ni usiku mkubwa kwangu mimi na kwa familia yangu baada ya kuitumikia klabu hii kwa maisha yangu yote, ila pia inaleta maana zaidi kwa mashabiki wa timu hii kwani wameonesha ukarimu na kunijali kwa muda wangu wote''

No comments:

Post a Comment