Friday, June 10, 2011

PELE ASEMA NEYMAR ANAHITAJI JUHUDI ZAIDI



Kinda nyota anaechipukia kutoka brazili NEYMAR ameonywa na gwiji la soka wa taifa hilo na duniakwa jumla PELE kuwa anahitaji juhudi zaidi ili kuweza kufuata nyayo zake na asijishughulishe na kucheza na mashabiki kwani wanaweza kumpotezea malengo yake.
Pia gwiji huyo hakusita kumfagilia nyotaa huyo kwa kusema anaweza kumpita nyota wa sasa wa Argentina Leonel Messi kwani anaonesha kuwa na uwezo mkubwa pamoja na kuwa na umri mdogo wa miaka 19.
NEYMAR anahusishwa na kuwaniwa na vigogo viwili vya soka barani ulaya CHELSEA na REAL MADRID huku CHELSEA wanaonekana kuwa na nafasi nzuri ya kumnyakuwa kwani wao ndio walioonesha nia ya kumnyakuwa nyota huyo tangu msimu uliomalizika hivi karibuni.
Uwezo wa nyota huyo unaonekana kuwa mkubwa hasa kutokana na kuwa na uwezo wa kutumia miguu yote miwili tofauti na MESSI.

No comments:

Post a Comment