Friday, June 10, 2011

.BARCELONA NA DILI LA FABRIGAS

BARCELONA NA DILI LA FABRIGAS

June 8, 2011

Klabu ya barcelona imetowa ofa ya kumpeleka mchezaji Thiago Alcantara katika klabu ya Arsenal kama miongoni mwa dili ya kutaka kumrejesha kikosini mchezaji Sesc Frbrigas ambaye anaonesha hana raha kikosini hapo huku akionesha nia ya kutaka kurejea katika miamba hiyo ya ulaya.
Katika mpango huo wa kumsajili Sesc Fabrigas itahusisha pesa ambazo Arsenal wanataka wapewe kiasi cha paundi milioni hamsini, lakini barcelona wanataka wakamilishe dili hilo kwa kubadilishana na Arsenal Thiago pamoja na pesa kama njia ya kuwashawishi arsenal kumtoa mchezaji wao huyo wa zamani alieondoka kikosini hapo akiwa kinda katika academy yao ya LAMASIA.
Mchezaji huyo ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Barcelona na Brazil Manzinho ameonekana kufuata nyayo za baba yake kutokana na kuonekana na kipaji cha hali ya juu tangu alipofika katika kikosi hicho ambaye amelelewa katika academy ya Barcelona ya LAMASIA lakini ameonekana kama amekata tamaa katika kupigania namba katika kikosi cha kwanza kutokana na kuwepo viungo mahiri katika klabu hiyo ambao ni XAVI na INIESTA ambao wametawala katika sehemu hiyo ya kiungo na Barcelona wanaona ni vizuri kumpeleka Arsenal ili aweze kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.

No comments:

Post a Comment