Friday, June 10, 2011

HISTORIA YA KLABU

VIKO PHARM FC

VIKOKOTONI PHARMACY FOOTBALL CLUB  ni klabu ya daraja la pili taifa ambayo imeanzishwa mwaka 2009 Zanzibar. Manager wa klabu hii Bwana Haji Ali Haji ambae ndio mmiliki wa klabu hii alikuwa na wazo la kuanzisha klabu ya mpira muda mrefu lakini malengo yake yalikuwa ni kuwa na timu ambayo itakuwa na uwezo wa kiushindani kitaifa na kimataifa pia kuweza kuuza wachezaji nje ya nchi, ndipo alipoamuwa kutafuta makocha ambao watakuwa na uwezo wa kufikia malengo hayo. mwaka 2009 alipata makocha wawili wazoefu ambao ni kocha mkuu Aley Mohammed Aley na kocha Msaidizi ambaye ni Said Muharram Dosi. makocha hawa ni makocha wazoefu kutokana na fani zao wote wakiwa tayari wamesha fundisha vilabu tofauti mjini Zanzibar kwani kocha Aley tayari alikwa kocha wa zamani wa TEMBO HOTEL na kocha Said alikuwa kocha wa zamani wa timu ya SMALL SIMBA. hawa ni makocha ambao wanauzoefu mbali na kufundisha pia walikuwa ni wachezaji wastaafu wa timu ya taifa ya zanzibar. Pia klabu hii inaundwa na viongozi wengine wawili ambao ni dactari wa timu Dr. Khamis na katibu wa timu ambaye ni bwana Hussein.
Timu inaundwa na wachezaji ishirini wengi wao wakiwa na umri kati ya miaka 18-23 ambao ni wachezaji  ambao wapo katika umri wanaoweza kufundishika na kuifanya timu kuweza kufikia malengo waliojipangia.
Pia makocha wa timuu hii ukiachia mbali uzoefu pia wamepata mafunzo mbali mbali ndani na nje ya nchi katika fani hii ya mpira wa kisasa na kutokana na hilo progarm za timu zinaendana sawa sawa na klabu yoyote ile duniani katika misingi ya wachezaji wa kulipwa duniani hivyo kuifanya kuwa klabu pekee Tanzania inayotegemewa kutoa wachezaji wengi nje ya nchi kucheza soka la kulipwa ulaya na sehemu nyengine duniani na kuifanya klabu kufikia malengo yake.
Mpaka sasa klabu haina mdhamini ila mmiliki ndio anaiendesha na tupo katika mchakato wa kutafuta wadhamini mbali mbali wa kuisaidia timu pamoja na wao wenyewe kujitangaza kupitia jezi zetu pamoja na website hii kwani program ya klabu ni kuhakikisha VIKOKOTONI FOOTBAL CLUB inafahamika duniani kote  hivyo tunakaribisha makampuni yote ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika klabu hii na tunawaahidi kutowaangusha na tutafanya kazi bega kwa bega kuhakikisha kuna manufaa kwa pande zote mbili 

No comments:

Post a Comment