Friday, June 10, 2011

MANCHESTER WAMSAJILI PHIL JONES


 MANCHESTER WAMSAJILI PHIL JONES

June 8, 2011

Klabu ya manchester united imemsajili beki wa blackburn Phil Jones kwa uhamisho unaokisiwa kufikia paundi millioni kumi na sita (16 ml pound).
mchezaji huyo ambaye anachezea timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 ameonekena leo mchana katika jiji la manchester united akifanyiwa vipimo na kusaini mkataba wa miaka mitano ambao utamuweka katika klabu hiyo mpaka mwaka 2016 alikuwa pia anawaniwa na klabu ya Liverpool lakini wekundu hao wa anfield wameshindwa na mashetani wekundu hao ambao wamelamba dume kwa kumsajili beki huyo.
Phil Jones ni beki ambaye msimu huu uliopita amecheza katika klabu yake hiyo kwa mafanikio makubwa huku akitikisa nyavu mara saba na kumfanya kuwa beki ambaye amefunga magoli mengi zaidi kwa msimu uliomalizika hivi karibuni na Mancheester United kutangazwa mabingwa wakiwa wamechukuwa ubingwa huo kwa mara ya kumi na tisa huku wakiweka historia ya kuwa klabu ambayo imebeba kombe hilo mara nyingi zaidi nchini England.
Awali Manchester United na Liverpool walikuwa wanachuanakatika kumsajili mchezaji wa sunderland handerson lakini wekundu hao wa Anfield wamefanikiwa kumsajili na hii inaonesha sir alex ferguson amelipiza kisasi kwa Liverpool kwa kusajili beki huyo.
Kutokana na kinachotokea sasa hivi ndani ya klabu ya Manchester United ni kuthibitisha ahadi ya kocha mkuu wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson kuwa anataka kukifanya kikosi hicho cha United kama cha Barcelona kwa kuwa na wachezaji wengi wa katika kikosi hicho kwani mpaka sasa yuko mbioni kufuata saini ya kiungo mshambuliaji wa Aston Villa Ashley Young ambaye yeye mwenyewe ameonesha nia ya kutaka kukipiga katika klabu hiyo

No comments:

Post a Comment